Image
Image

Prince William amesema ameanza kupata na hemwa hemwa juu ya mchezo wa fainali ya FA.


Mwana wa kifalme wa Uingereza Prince William amesema kuwa, ameanza kupata hemwa hemwa juu ya mchezo wa fainali ya FA itayopigwa hapo kesho kati ya Arsenal dhidi ya Aston Villa.
Prince Willium ambaye ni shabiki wa mkubwa wa Aston Villa, anasema atakuwepo katika dimba la Wembley kutazama mpambano huo huo pamoja na kukabidhi kombe kwa timu itakayoibuka kidedea. " nina wasiwasi na hofu" alisema Prince.
Mwana huyo wa kifalme ambaye ndiye rais wa chama cha soka cha Englan FA, pia ameiambia BBC juu ya matumaini yake ya kuona wanawe wakifuata nyayo zake za kuwa mashabiki wa Aston Villa. Ushabiki wa Prince William kwa timu hiyo, umeanza tokea akiwa shuleni kwakuwa aliamini kuishabikia Aston Villa kungemfanya awe na hisia nzuri, japo ametanabaisha kuwa marafiki zake walikuwa ni Mashabiki wa Manchester Utd na Chelsea
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment