Image
Image

Rais mpya wa Nigeria Muhamadu Buhari ameapishwa rasmi kushika nafasi hiyo.


Rais mpya wa Nigeria Muhamadu Buhari leo ameapishwa kushika nafasi hiyo kufuatia kushinda kwake katika  uchaguzi mkuu dhidi   Goodluck Jonathan aliyekuwa madarakani katika kiti hicho cha urais wakati wa uchaguzi huo.
Saa chache kabla ya kufanyika kwa hafla ya kumuapisha Jenerali bBuhari kuongoza taifa hilo la nigeria yalifanyika makabidhiano ya kuongoza taifa hilo kati ya rais aliyeshindwa katika uchaguzi mkuu  uliofanyika mwezi March Bw.Goodluck  Jonathan na rais huyo mteule.
Katika mkesha wa kusubiri kuapishwa kwake huku burudani zikitawala katika viunga mbali mbali vya nchi hiyo huku wananchi wa Nigeria wakielezea kuwa wanamatumaini makubwa kuwa kiongozi huyo mpya kuwa atamaliza mataifa yanayolibili taifa hilo.
Wachambuzi wa masuala ya siasa nchini Nigeria wamesema kuwa rais Buhari anakabiliwa na jukumu kuu la kuhakikisha anatokomeza kikundi cha kigaidi cha kiislamu cha Boko haramu sambamba na kuwaokoa mateka mbalimbali wanaoshikiliwa na kikundi hicho.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment