Image
Image

News Alert:Wakimbizi 31 kutoka Burundi waripotiwa kufariki kwa ugonjwa wa Kipindupindu Kigoma.



Wakimbizi 31 kutoka Burundi wameripotiwa kufariki Dunia kutokana na ugonjwa wa Kipindupindu ulioibuka wiki mbili zilizopita katika kituo cha mapokezi katika Kijiji cha Kagunga Wilayani Kigoma.
Mkuu wa kambi ya wakimbizi Nyarugusu katika wilaya ya Kasulu mkoani humo,  SOSPETER  BOYO akitoa taarifa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, amesema vifo hivyo vimetokea katika kijiji cha Kagunga na katika kambi ya wakimbizi ambako walifikishwa wakiwa tayari na maambukizi.


Amesema licha ya kwamba hivi sasa kuna wagonjwa 46 wanaoendelea na tiba, lakini wamefanikiwa kuudhibiti ugonjwa huo kutokana na kuimarisha huduma za afya kwa kushirikiana na mashirika yanayotoa huduma kwa wakimbizi.
Kwa upande wake , Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, MATHIAS CHIKAWE amesema inafanya jitihada kuhakikisha wakimbzi ambao kwa sasa wanaishi katika kambi ya wakimbizu wenzao kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo  wanapatiwa eneo lao ili kuepusha msongamano ambao unaweza kuchangia mlipuko wa magonjwa mbalimbali.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment