Image
Image

Azam kutumia 'wakaabenchi' Kagame Cup.

Uongozi wa Azam FC umesema timu yao itashiriki michuano ya Kombe la Kagame bila nyota wake wengi wa kikosi cha kwanza ambao wanazitumikia timu zao za taifa.

Saad Kawemba, Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Azam FC, alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa hawajaipa kipaumbele michuano hiyo kwa sababu nguvu kubwa wameiweka katika kusuka kikosi kwa ajili ya msimu wa 2015/16 wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na Kombe la Shirikisho barani Afrika mwakani.

Alisema kikosi chao kitashiriki Kombe la Kagame, lakini michuano hiyo ni sehemu ya maandalizi yao kwa ajili ya msimu mpya wa VPL.

Alisema sehemu kubwa ya kikosi chao itaundwa na wachezaji vijana na wakubwa wachache ambao hawakuitwa kwenye timu zao za taifa ili kutoa nafasi ya kupumzika kwa wale waliokuwa wanazitumikia timu zao za taifa.

“Maandalizi yanaendelea vizuri, tunaingia katika michuano mikubwa ya Kombe la Kagame tukiwa tumefanya maandalizi ya wiki tatu tu. Katika sayansi ya michezo hatuko 'fiti', ili uwe vizuri, lazima ufanye mazoezi walau kwa wiki saba hadi nane," alisema Kawemba na kueleza zaidi:

"Tutatumia wachezaji wachache wa kikosi chetu cha kwanza kwa sababu tutatoa mapumziko kwa wachezaji walioitwa kuzitumikia timu zao za taifa. Kumbuka Azam ina wachezaji 12 Taifa Stars na hawajapata muda wa kutosha wa kupumzika tangu kumalizika kwa msimu uliopita.

“Kombe la Kagame kwa kweli siyo ‘priority’ (kipaumbele) yetu, tunaomba radhi kwa waandaaji wa mashindano hayo. Tutacheza, lakini tutashiriki kama sehemu ya maandalizi kwa ajili ya msimu ujao."

Aggrey Morris, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Brian Majwega, Salum Abubakar 'Sure Boy' na Frank Domayo ni miongoni mwa nyota wa Azam FC watakaoikosa michuano ya Kombe la Kagame itakayofanyika jijini Dar es Salaam mwezi ujao.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment