Image
Image

Malinzi: TFF itamwaga pesa vituo 27 Tanzania.

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, amesema mamlaka hiyo ya soka nchini itakuwa inatoa fedha na misaada mbalimbali kusaidia vituo 27 vya kukuza na kuendeleza vipaji vya michezo ambavyo kila mkoa umeagizwa kujenga.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya juzi, Malinzi ambaye yupo mjini hapa kwa ziara na timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 15, alisema kuwa kila mkoa (chama cha soka cha mkoa husika) nchini umeagizwa na shirikisho hilo kuwa na kituo kimoja cha michezo ambacho TFF itahakikisha inakisaidia kuwa na walimu wa kutosha, vifaa na mahitaji mengine.

Malinzi pia alisisitiza kuwa shirikisho hilo litasimamia ipasavyo kanuni ya kila timu ya ligi kuu nchini kuwa na timu ya vijana itakayokuwa inacheza mechi za utangulizi ikiongozwa na kocha mwenye taaluma stahiki. 

Malinzi aliongeza kuwa ya timu ya taifa ya vijana iliyopiga kambi jijini hapa itafanya ziara katika mikoa mbalimbali nchini. 

Alisema mwezi ujao itaelekea visiwani Zanzibar, Agosti itakuwa Mwanza, Septemba itakuwa Morogoro na Oktoba itakuwa Arusha huku ikiendelea kuchujwa na Desemba itafanya ziara katika nchi za Malawi, Zambia, Botswana na Afrika Kusini kabla ya kuelekea Kaskazini mwa Afrika.

Malinzi alisema wanaamini maandalizi hayo yatatoa timu bora ya vijana itakayoiwakilisha vyema Tanzania katika michuano ya kimataifa ikiwamo Olimpiki na fainali za Kombe la Dunia 2026.

"Ni vigumu sana timu kushiriki mashindano ya Kombe la Dunia kwa maandalizi ya muda mfupi. Maandalizi tunayofanya tunaamini yatatusaidia kuimarisha timu yetu kwa ajili ya miaka ijayo,” alisema Malinzi.

Katika ziara yake jijini hapa, timu ya taifa ya vijana ya U15 ilicheza mechi ya kirafiki na kushinda 3-0 dhidi ya timu ya Mbeya Combine ya umri huo mwishoni mwa wiki.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment