Image
Image

JK kuvunja Bunge Julai 9.

Hatimaye imebainika kwamba Bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, litafikia ukomo wake Julai 9, mwaka huu.

Hadi kufikia mwisho wa uhai wake, Bunge hilo lililoongozwa na Spika Anne Makinda 
(Pichani),  na Naibu Spika Job Ndugai, litakuwa limefanya mikutano 20  huku vikao vya mwisho vikiwa ni 38.

Ratiba ya nyongeza iliyotolewa jana na ofisi ya Bunge baada ya kikao cha Kamati ya Uongozi, ilionyesha kuwa Rais Jakaya Kikwete atalivunja Bunge hilo baada ya kulihutubia.

Pamoja na tukio hilo la kihistoria, Bunge limejadili miswada mbalimbali ikiwamo (iliyopitishwa) ya sheria ya fedha ya mwaka 2015, sheria ya vituo vya pamoja mipakani ya mwaka 2015 na sheria ya kufuta sheria ya benki ya Posta ya mwaka 2015.

Aidha, baada ya maoni ya wadau wa habari, muswada wa haki ya kupata habari ambao ulikuwa ujadiliwe Juni 27, mwaka huu, baada ya kusomwa kwa mara ya kwanza, uliondolewa bungeni hadi serikali ijayo.

Miswada inayoendelea kujadiliwa ni muswada wa sheria ya masoko ya bidhaa wa mwaka 2015, muswada wa sheria ya kuwalinda watoa taarifa za uhalifu na mashahidi wa mwaka 2015.

Mingine ni muswada wa sheria ya Petroli wa mwaka 2015, muswada wa sheria ya usimamizi wa mapato ya mafuta na gesi wa mwaka 20q5, muswada wa sheria ya uwazi na uwajibikaji katika tasnia ya uchimbaji Tanzania ya mwaka 2015.

Ratiba hiyo imeonyesha kuwa muswada mwingine nj wa sheria ya Tume ya walimu wa mwaka 2015.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment