Image
Image

Nec yapokea maombi ya waangalizi wa uchaguzi.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imepokea maombi kutoka taasisi za ndani zilizoomba kuwa waangalizi wa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba  25, mwaka huu.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Nec, Julius Malaba alisema maombi ya waangalizi wa ndani wa uchaguzi yalishapokewa huku mchakato wa kuwateua wanaostahili ukiendelea kufanyika.

“Waaangalizi wa ndani wa uchaguzi wameshatuma maombi yao  na mchakato wa kuzipata taasisi zenye sifa ya kuwa waangalizi unaendelea muda utakapofika zilizochaguliwa zitatangazwa,” alisema.

Kuhusu waangalizi wa nje, Malaba alisema jukumu hilo linatekelezwa na  Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa na kwamba jumuiya kadhaa zimeshatumiwa mialiko.

“Unapomwalika mtu ama taasisi haimaanishi lazima aje, uamuzi wa kuja ama kutokuja unabaki kuwa ni hiyari ya mhusika,” alisema.

Hata hivyo, jitihada za kumpata  Waziri wa wizara hiyo, Bernard Membe, kuzungumzia suala hilo hazikufanikiwa kutokana na simu yake ya kiganjani kutopatikana.

Membe ni miongoni mwa mawaziri katika serikali ya Rais Jakaya Kikwete, wanaoomba kuteuliwa na CCM ili wawanie urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Kuhusu changamoto zinazotokana na uandikishaji wapiga kura kwa mfumo wa BVR, Malaba alisema Nec mchakato huo umeahirishwa kwa mikoa kadhaa ukiwamo Dar es Salaam ili vifaa vilivyokusanywa katika mikoa ambayo mchakato umemalizika viweze kutosheleza idadi ya wakazi wake.

“Tumejipanga kuhakikisha wakazi wote wa Dar es Salaam wanaandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura ndio utaona tumesogeza mbele siku ya uandikishaji ili kukusanya vifaa vyote vilivyotumika katika mikoa mingine kuendana na idadi ya watu,” alisema.

Pia, Malaba alisema hadi sasa hakuna tarehe mahususi ya mwisho ya kuzaliwa kwa mpiga kura mwenye sifa ya kujiandikisha, isipokuwa ni atakayekuwa na umri wa miaka kuanzia 18 ifikapo Oktoba 25, 2015.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment