Image
Image

Polisi mmoja ajeruhiwa kwenye shambulizi lililotekelezwa katika mji mkuu wa Bujumbura.


Shambulizi limeripotiwa kutekelezwa katika eneo la Jabe lililoko mjini Bujumbura ambapo polisi walikuwa wakifanyia ukarabati barabara zilizoharibiwa katika maandamano ya ghasia nchini Burundi.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na msemaji wa idara ya polisi, jamaa mmoja alilipua kilipuzi kwenye barabara hiyo na kusababisha polisi mmoja kujeruhiwa.
Maelezo zaidi yanaarifu kwamba kulisika milio ya risasi baada ya shambulizi hilo kutekelezwa.
Mshambuliaji huyo ameripotiwa kutoroka baada ya kulipua kilipuzi hicho barabarani.
Jabe ni mojawapo ya maeneo ya mji mkuu wa Bujumbura nchini Burundi ambayo maandamano ya ghasia dhidi ya rais Nkurunziza yalifanyika kwa muda mrefu.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment