Image
Image

Wananchi waeleza hofu ya siku zilizobaki za uandikishwaji katika daftari la mpiga kura kutokidhi kiu yao.

Zikiwa zimesalia siku chache za kukamilishwa kwa uandikishaji wa Daftatri la wapiga kura kwa mfumo wa BVR katika jiji la Dar es Salaam bado wananchi wameeleza hofu ya siku hizo kutotosheleza kwa madai ya kasi ndogo ya mashine na zingine kuharibika mara kwa mara hali iliyoibua kundi la wajasiria mali wanaowahi kujiandikisha kupata namba na kisha kuziuza kwa kati ya shilingi el 7 hadi kumi.
Wakizungumzia hali hiyo baadhi ya wakazi wa mpiji-magohe nje kidogo ya Dar es Salaam wamesema hali hiyo inachagizwa na muamko mkubwa wananchi kujiandikisha huku mashine zikiwa hazikidhi mahitaji ya wakazi wa jiji ambao asilimia kubwa hutegemea kipato cha kila siku ambapo kwa sasa  mtu anatumia siku Tau  hadi hadi Tano kujiandikisha .
Vijana ambao walijipambanua kuwa itakuwa mara ya kwanza kupiga kura wa dhamira ya kuondoa au kufuta dhana iliyokuwa ikitawala majukwaa ya kisiasa kuwa vijana wanafika mikutanoni lakini hawapigi kura huku wakilaani makundi yanayofanya biashara ya kuuza namba katika vutuo vya kupigia kura.

TAMBARARE HALISI katika pita pita yake imebaini baadhi ya maofisa wa tume wakipakia mashine kwenye bodaboda kutoka katika baadhi ya vituo kwa madai ya kuharibika huku mkurugenzi wa manispaa ya kinondoni ambaye pia ni msimamizi wa zoezi hilo Eng. Musa Nati akikiri changamoto kadha kwa maelezo ya kuwa tume ya taifa ya uchaguzi NEC itatoa mwelekeo kulingana na mahitaji ya wakazi katika kuhakikisha kila mwenye sifa ya kujiandikisha anafanya hivyo.

Aidhaa kwa mwaka huu wa 2015 idadi ya uandikishwaji wananchi katika daftari la Mpiga kura imeonekana kuongezeka maradufu,huku watu wengine wakiamka usiku wa manane kwa lengo la kuwahi namba ili kupata kitambulisho kitakacho fanya awe na sifa ya kupiga kura ifikapo Oktoba mwaka huu katika uchaguzi mkuu wa kuchagua Madiwani,Wabunge hadi ngazi ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment