Mkuu wa mkoa wa Iringa Bibi AMINA
MASENZA ametoa changamoto hiyo wakati wa makabidhiano ya nyumba mbili za walimu
na nyumba moja ya askari polisi katika vijiji vya Kipera na Idodi katika tarafa
ya Idodi na Tungamalenga katika tarafa ya Pawaga zenye thamani ya zaidi ya
shilingi milioni mia mbili zilizojengwa kwa ushirikiano wa hifadhi hiyo na
wananchi wa tarafa za Idodi na Pawaga na hifadhi hiyo.
Kwa upande wake, Mhifadhi Mkuu wa
Hifadhi ya Taifa ya Ruaha Dakta CHRISTOPHER TIMBUKA amesema mradi wa ujirani
mwema umesaidia ujenzi wa miradi mbalimbalimbali ya m aendeleo kwa lengo la
kujenga u husiano kati ya hifadhi na wananchi wanaoizunguka .
Naye Ofusa Mtendaji wa kijiji cha
Kipera Bwana JOSEPH KALINGA amesema kijiji hicho kilitumika kama kama maficho ya majangili waliokuwa wa
kiua tembo katika Hifadhi ya Taifa ya
Ruaha, lakini kutokana na elimu ya uhifadhi inayotolewa kupitia mradi wa
ujirani mwema, wananchi wamebadilika na kushiriki katika shughuli za uhifadhi
kwa kuwalinda wanyama wakiwemo tembo wa Ruaha.
0 comments:
Post a Comment