Chama cha walimu nchini Tanzania CWT kimeitaka
serikali kukamilisha madai ya walimu hadi ifikapo September mwaka huu.
Akizungumza na wanahabari mapema leo Rais wa chama hicho
Bwana GRATIAN MUKOBA amesema kuwa serikali imekuwa ikupuuza madai ya walimu hao
kwa muda mrefu sasa ambapo amesema kuwa mnamo agost tatu mwaka huu
serikali kupitia wizara ya elimu ilikutana na walimu ili kujadili mambo
mbalimbali ikiwemo muundo mpya wa kazi na malipo ya walimu lakini bado serikali
haikutoa majibu ya moja kwa moja kuwa itatatua changamoto hizo lini .
Aidha Bwana MUKOBA amesema kuwa sheria ya malipo ya walimu
katika kada mbalimbali inaelekeza kuwa mishahara iendane na posho ambapo hadi
kufikia leo hakuna posho yoyote iliyotolewa kwa mwalimu yeyote hali
inayopelekea deni la walimu kufikia billion tano hadi sasa
Sambamba na hilo MUKOBA amebainisha kuwa kuna baadhi ya
wastaafu ambao hawajalipwa malipo yao tangu mwezi wa nane mwaka jana hali
inayowafanya wastaafu hao kubaki omba omba katika maeneo mbalimbali nchini.
Hata hivyo Bwana Mukoba ameongeza kuwa ni lazima serikali
itenge hela zinazotosha kulipa madeni yote ya walimu ili kuhakikisha kuwa
walimu wanarudisha ari na muamko wa utekelezaji wa majukumu yao ya kujenga
taifa na kuboresha mazingira yao ya utoaji wa elimu.
Katika hatua nyingine MUKOBA amesema kuwa mnamo mwezi ujao
kutakuwa na mkutano mkuu wa walimu hao ambao pamoja na mambo mengine mada kuu
watakuwa wakiangalia serikali imetekelezaje madai hayo waliyoyatoa kabla ya
kujadili kwa kina mambo ya kufanya kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.->Kujua zaidihttp://habari24.blogspot.com

0 comments:
Post a Comment