Image
Image

Magufuli ahofia maamuzi magumu kwa watanzania.

Mgombea wa kiti cha urais kupitia chama cha mapinduzi CCM Dr.John Pombe Magufuli amewataka watanzania kutofanya kile kinachoitwa maamuzi magumu kama libya ilivyofanya kwa kumuondoa madarakani rais wa nchi hiyo Muamary Ghadaffi na hii leo wamegeuka wakimbizi ndani ya nchi yao la sivyo wafanye mabadiliko kama china ilivyofanya katika chama cha Kikomunist cha kufanya mabadiliko ndani ya chama na hivyo na hii leo china imekuwa miongoni Mwa nchi ya kwanza kiuchumi duniani.

Baada ya ufafanuzi huo kuhusu habari ambazo simesambazwakatika mitandao ya kijamii Dr.Magufuli ambaye amepewa na wananchi jina la mzee wa kazi akaanza ziara yake ya kusaka ridhaa ya watanzania kiongoza Tanzania mkoani Njombe ambapo amewataka watanzania kupuuza kile kinachoitwa mabadiliko kwa kuwa hata Libya ilifanya mabadiliko ya kukurupuka kutokana na utamu wa lugha za wapinzani wake na hii leo wananchi hao wa Libya wanahangaika na kuwataka kumpa fursa ya urais ili afanye mabadiliko ya kimfumo na kiuchumi taifa lisonge mbele kimaendeleo.

Aidha Dr.Magufuli akizungumza kwa sauti ya kumaanisha kwa dhati kile anachokisema amewataka watanzania kumwamini kumpa ridhaa ya kuwa rais na kwamba Tanzania itaendeshwa bila ya ubaguzi na maendeleo ya kweli yataonekana.

Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa Mh.Dr.Harrison Mwakyembe amewaeleza watanzania kuwa Tanzania haitaki viongozi wa maamuzi magumu na badala yake inamtaka kiongozi mwadilifu atakayesimamia rasilimali za taifa kwa usawa na haki bila uonevu na ambao wanapaswa kuaminiwa na wakipewa madaraka hawatadokoa kwa manufaa yao rasilimali za taifa.

Katokana na kile kinachoneka kuwa sera na kampeni za kistaarabu zinazofanywa na Dr.Magufuli baadhi ya wananchi waliokuwa katika vyama vya upinzani wamerejesha kadi zao na kujiunga na CCM kwa kile walichodai ni kuchoshwa kutumika kama ngazi na viongozi wa CHADEMA.

Jumapili ya August 30 ziara za Dr.Magufuli kusaka ridhaa ya watanzania kuiongoza Tanzania itaendelea mkoani Ruvuma.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment