Image
Image

Mkoa wa Kagera bado unakabiliwa na ongezeko la ajali za Barabarani.


Wananchi wakiwa wamejipanga msururu kila mmoja kutaka kuona kilichotokea baada ya gari hizo kugongana na kusababisha ajali(Picha na Maktaba).
Pamoja jitihada za jeshi la Polisi Mkoani Kagera za kubuni mikakati ya kukabiliana na ajali za barabarani kwa kushirikiana na idara nyingine za serikali na wadau mbalimbali  bado  mkoa huo unaendelea kukabiliwa na ongezeko la ajali  ambazo hutokea na wakati mwingine husababisha  vifo na majeruhi.
Akizungumza wakati wa  maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama ambayo katika Mkoa wa Kagera  yamefanyika Wilayani Misenyi,  Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani humo, WILLIAM MKONDA wakati akitoa takwimu za hali ya ajali na mambo yanayosababisha ajali katika mkoa huo.
Amesema katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Juni mwaka huu idadi ya ajali zilizotokea Mkoani Kagera na kusababisha vifo na majeruhi kuwa imeongezeka ikilinganishwa  na ajali zilizotokea mwaka jana katika kipindi hicho.
Kwa upande wake,  OBEDI ILOMO,  Katibu Tawala wa Wilaya ya Misenyi ambaye alikuwa mgeni rasmi  katika maadhimisho hayo,  amewataka watumishi wa umma waliopewa dhamana kusimamia sheria na kanuni za usalama barabarani kutekeleza majukumua yao kwa uadilifu.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment