Katibu Mkuu wa UN Ban Ki-moon, amemhimiza Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir kutia saini mkataba wa amani kabla ya muda wa siku 15 walizopewa kutimia.
Kiir alikataa kutia saini mkataba wa amani siku ya Jumatatu na kuomba apewe muda wa siku 15 zaidi kabla ya kutoa uamuzi wa mwisho.
Hapo awali, mazungumzo ya mkataba wa amani yalikuwa yamewekewa tarehe ya mwisho na jumuiya ya kimataifa kuwa Agosti 17.
Baada ya mkutano kufanyika siku ya Jumatatu katika mji mkuu wa Addis Ababa nchini Ethiopia, kiongozi wa kundi la waasi ambaye ni makamu wa rais wa zamani wa Sudan Kusini Riek Machar, alitia saini mkataba wa amani.
Serikali ya Sudan Kusini imetangaza kwamba itarudi tena Addis Ababa baada ya siku 15, kwa ajili ya kutamatisha mazungumzo hayo ya mkataba wa amani.


0 comments:
Post a Comment