Image
Image

Jeshi la Burkina Faso limechukua udhibiti wa kambi zote za kijeshi zilizokuwa zinakaliwa na kikosi maalum cha walinzi wa rais.

Jeshi la Burkina Faso limechukua udhibiti wa kambi zote za kijeshi zilizokuwa zinakaliwa na kikosi maalum cha walinzi wa rais kilichovunjwa mwishoni mwa wiki na kutakiwa kusalimisha silaha lakini wakakataa kufanya hivyo.
Haijafahamika kama kuna madhara yoyote yalijitokeza katika kukuchukuliwa kambi kubwa ya walinzi hao lakini mapema milio ya risasi na milipuko ilisikika na moshi kutapakaa kutoka eneo la kambi hiyo.
Taarifa zinasema kiongozi wa mapinduzi hayo ya mapema mwezi huu Jenerali Gilbert Diendere ambaye haifahamiki alipo alitaka kikosi chake kusalimu amri ili kuepuka umwagaji damu.
Serikali ya mpito chini ya Rais MICHEL KAFANDO imesema kwa jumla imefanikiwa
kusambaratisha vikosi vya vya ulinzi vilivyokuwa vitiifu kwa Rais wa zamani wa nchi hyo,
Bwana Blaise Compaore na Jenerali Diendere.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment