Image
Image

Mapigano makali yanaendelea katika mji wa Kunduz kaskazini mwa Afghanistan.


Mapigano makali yanaendelea katika mji wa Kunduz kaskazini mwa Afghanistan siku moja
baada ya majeshi ya serikali kuanzisha oparesheni ya kuurejesha tena mji huo uliotekwa
na wapiganaji wa Taliban.
Mapema mashambulio mawili ya anga yaliyofanywa na Marekani yalizuia jaribio la
wapiganaji hao kukamata uwanja wa ndege wa Kunduz, ambao ni ngome ya jeshi la nchi hiyo
na mji mkuu wa jimbo la mpakani na Pakistan.
Kutekwa kwa mji huo ni ushindi mkubwa wa wapiganaji hao tangu mwaka 2001 wakati utawala
wa Taliban ulipoondolewa madarakani kufuatia uvamizi ulioongozwa na Marekani.
Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema ina imani kuwa jeshi la Afghanistan litaukomboa mji
huo wa Kunduz kaskazini mwa nchi hiyo uliotekwa na wapiganaji wa kikundi cha Taliban.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment