Kutokana na uvumi mwingi ama kile kilichokuwa
kikionekana kwamba pengine huenda Bi.Makinda ambaye alikuwa ni Spika wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Bunge la kumi kwamba huenda angewania
tena nafasi hiyo kwa kipindi hiki cha uongozi mpya chini wa Dk.Magufuli amesema
hana mpango huo kuwania bunge la Kumi na Moja na wala hajathubutu kwenda
kuchukua fomu kwani kipindi alichofanya kinatosha.
Hata hivyo baada ya CCM kufungua pazia la watu
wanaotaka kuwania nafasi za Uspika na unaibu Spika wa Bunge la jamhuri ya
muungano wa Tanzania kuchukua fomu hizo ni zaidi ya watu kumi kutoka CCM tayari
wamejitokeza.
Katika kujitokeza huko ni pamoja na aliyewahi kuwa
waziri wa uchukuzi nchini Tanzania Samuel Sitta ambaye pia aliwahi kuwa Spika
wa Bunge la Tisa na Mwaka 2010 alichukua tena fomu hiyo kuwania nafasi hiyo
lakini aligonga mwamba baada ya chama hicho kuweka kigezo cha mgombea
Mwanamke,hivyo nafasi hiyo kuchukuliwa na Anne Makinda.
Mbali na sita Pia wapo waliochukua fomu akiwemo
Dk.Emmanuel Nchimbi,aliwahi kuwa waziri wa mambo ya ndani,Leonce Mulenda,Costa
Mahalu aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini italia,Balozi Philip
Marmo,Simoni Rubugu,Gosbert Blandes
aliyewahhi kuwa mbunge Karagwe katika bunge lililopita,Didas Masaburi na Dk.Kalokola Muzamili hao
wakiwa tu ni baadhi.

0 comments:
Post a Comment