Lebanon inaombole za vifo vya watu 43 ambao wameuawa kusini mwa mji mkuu
Beirut katika milipuko ya mabomu iliyolilenga kundi la wanamgambo wa
Hezbollah.
Milipuko hiyo imetokea katika mtaa wa shughuli nyingi za biashara wa
Burj al-Barajneh, ambako kundi la Hezbollah ambalo wafuasi wake wengi ni
wa madhehebu ya Shia, linao umaarufu mkubwa.
Shirika la msalaba mwekundu limesema mbali na watu 43 waliouawa, wengine
karibu 240 wamejeruhiwa katika milipuko hiyo, wengi wakiripotiwa kuwa
katika hali mahtuti. Mashambulizi hayo yanakumbushia kampeni dhidi ya
Hezbollah kati ya mwaka 2013 na 2014 kama ulipizaji kisasi kwa uamuzi wa
kundi hilo kuunga mkono kijeshi serikali ya Syria dhidi ya makundi ya
waasi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Haya ni mashambulizi makubwa zaidi kuwahi kudaiwa kutekelezwa na kundi
la dola la kiislamu nchi Lebanon, na lenye umwagaji mkubwa wa damu tangu
kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya mwaka 1975 na 1990.
Hivi leo familia zilijianda kuondoa miiili ya wapendwa wao kutoka
hospitalini huku nchi hiyo iitangaza siku ya kitaifa ya maombolezo
ambayo imetangazwa na waziri mkuu Tammam Salam.
Shule zimefungwa kwa siku ya leo,huku wanasiasa wa pande zote wakishutumu mashambulizi hayo.
Milipuko hiyo ilisikika karibu na soko lililo karibu na watu masikini la
watu wa madhehebu ya Shia huku damu ikitapakaa kwenye sakafu na maduka
yaliyo karibu .
Jeshi la nchi hiyo limesema mashambulizi hayo yalitekelezwa na watu
wawili wa kujitoa mhanga,na mwili wa mtu wa tatu aliyejitoa mhanga
ambaye bomu lake halikulipuka, silaha yake ilikutwa katika eneo la
mlipuko wa pili.
Lakini dola la kiislamu limetoa kauli tofauti kwenye taarifa yake kwenye mtandao wakidai kuhusika na mashambulizi hayo.
Taarifa yao imesema na hapa ninanukuu "wanajeshi wetu wa kiislamu
walilipua vilipuzi vilivyokuwa vimefungwa kwenye piki piki mjini.Baada
ya walioasi kukusanyika katika eneo hilo mmoja wa wanajeshi wetu
alilipua kilipuzi katikati yao " mwisho wa kunukuu.
Taarifa hiyo haikuelezea kuhusika kwa Hezbollah katika nchi jirani ya
Syria ambayo eneo lake kubwa linadhibitiwa na dola la kiislamu la
IS,badala yake limetumia klugha ya mrengo wa kidini yenye kubeza
madhehebu ya Shia.
IS ambalo ni kundi la madhehebu ya Sunni huwachukulia watu washia na
waislamu wengine wasiokubali tafsiri yake ya dini ya kiislamu, kama
waasi wa dini.
Taarifa hiyo haikuweza kuthibitishwa mara moja ,lakini ilifuata
utaratibu wa kawaida wa madai ya kuhusika kwa kundi la dola la kiislamu
na kusambazwa kwenye mitandao ya makundi ya kigaidi.
Matangazo ya televisheni nchini Lebanon yaliangazia mashambulizi hayo .
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki moon aliyalaani mashambulizi hayo
huku akitaka vikosi vya usalama vya Lebanon kutoyaruhusu kuvuruga hali
ya utulivu nchini humo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment