Watu kadha
wameuawa kwenye shambulio la bomu na risasi katika mji mkuu wa Somalia
Mogadishu.
Walioshuhudia
wamesema wameona moshi ukitanda juu angani kutoka eneo la shambulio na kwamba
watu wengi wamejeruhiwa
Shirika la
habari la Reuters linasema watu watatu wamefariki.
Shambulio
lilianza kwa ufyatuaji wa risasi na kisha bomu likalipuka polisi walipowasili,
afisa wa polisi ameambia shirika la habari la AFP.
Haijabainika
ni nani aliyehusika kwenye shambulio hilo.
"Wengi
wa waathiriwa ni raia,” afisa wa polisi Ahmed Abdiweli ameambia AFP.
Gavana wa
eneo Husayn Ali Wehliye ni mmoja wa waliojeruhiwa, na amepata majeraha madogo
kwa mujibu wa vyombo vya habari Somalia.
Kundi la
wapiganaji wa Kiislamu la Al-Shabab limetekeleza mashambulio kadha wiki za
karibuni.
Majuzi
lilisema lilihusika kwenye shambulio katika hoteli moja mwezi uliopita ambalo
liliua watu 15 Mogadishu.
0 comments:
Post a Comment