Mreno huyo alifutwa kazi baada ya The Blues kushinda
mechi tisa kati ya 16 za kwanza Ligi ya Premia msimu huu.
“Hataenda likizoni, hajachoka, hahitaji likizo,” taarifa
kutoka kwa wakala anayemwakilisha Mourinho imesema.
“Ana matumaini sana na tayari anaganga yajayo.”
Mourinho alijiunga na Chelsea kwa mara ya pili Juni 2013
na msimu uliopita akawaongoza kushinda Ligi ya Premia na Kombe la Ligi.
Hata hivyo Chelsea wamehangaika sana msimu huu.
"Jose Mourinho ana furaha kwamba alirejea Chelsea
kwa sababu aliweza kuwapa mashabiki taji jingine la Ligi ya Premia, ligi ambayo
hawakuwa wameshinda kwa miaka mingi,” taarifa ya Mourinho imesema.
“Anajivunia sana kushinda vikombe vinane akiwa Chelsea na
anawashukuru mashabiki kwa muunga mkono vipindi hivyo viwili alikuwa katika
klabu hiyo.
"Wakati wa maisha yake ya ukufunzi, Jose wakati
mwingine amekuwa akiamua kuondoka katika klabu, lakini ni Chelsea pekee ambako
klabu iliamua anafaa kuondoka.”
Chelsea watacheza mechi yao ya kwanza bila Mourinho
Jumamosi, nyumbani dhidi ya Sunderland.
0 comments:
Post a Comment