Asilimia 62% ya wakazi wa jimbo la Handeni wameshindwa
kujitokeza kupiga kura wakidai kuwa tayari wameshajua kuwa mgombea ubunge kwa
tiketi ya CCM ataibuka mshindi kufuatia wagombea nafasi za ubunge kwa tiketi ya
chama cha wananchi CUF na chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kushindwa
kuafikiana kusimamisha mgombea mmoja.
Katika kinyang'anyiro hicho msimamizi wa uchaguzi jimbo la
Handeni mji amemtangaza mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM Mheshimiwa Omary
Abdalla Kigoda kuwa mshindi baada ya kupata kura 10,315 akifuatiwa na shundi
aidan wa CUF alipata kura 2415 na nafasi ya tatu ikishikiliwa na mgombea ubunge
kwa tiketi ya chadema Daud Lusewa aliyepata kura 648.
Kwa upande wake msimamizi wa uchaguzi jimbo la handeni
mji Bwana Keneth Haule amesema jumla ya wapiga kura walikuwa 38,610 lakini
walijitokeza kupiga kura walikuwa 13,591.
0 comments:
Post a Comment