Mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abramovich
amekutana na bodi ya klabu hiyo kujadili hatima ya meneja wa klabu hiyo Jose
Mourinho.
Hii ni baada ya klabu hiyo kuandikisha matokeo
mabaya sana msimu huu, matokeo ya karibuni zaidi yakiwa kuchapwa 2-1 na
Leicester ligini Jumatatu.
Hiyo ilikuwa mara ya tisa kwa Chelsea kushinda Ligi
ya Premia katika mechi 16 na sasa wamo alama moja pekee juu ya eneo la
kushushwa daraja.
Haijabainika iwapo Mourinho, 52, bado atakuwa kwenye
usukani wakati wa mechi kati ya The Blues na Sunderland Jumamosi uwanjani
Stamford Bridge.
Abramovich alitangaza kwamba bado alikuwa akimuunga
mkono Mourinho Oktoba lakini matokeo hayajaimarika.
Abramovich na wenzake uongozini Chelsea wamekuwa
wakimuunga mkono meneja huyo lakini kuna kizungumkuti cha ni hadi lini
watasubiri klabu hiyo iimarike.
Tatizo jingine ni kwamba kwa sasa hakuna meneja
msifika ambaye hana kazi na anaweza kuitwa upesi kujaza pengo.
Carlo Ancelotti ambaye hana kazi tayari alikuwa
Chelsea awali na akafutwa.
Meneja wa Bayern Munich Pep Guardiola na Diego
Simeone Atletico Madrid bado wana majukumu kwa sasa.
Hili limepelekea uvumi kwamba sasa huenda Chelsea
ikarudi tena kwa Guus Hiddink kwa mkataba wa muda.
Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 69 alishikilia
usukani kwa muda Chelsea mwaka 2009 na kuongoza klabu hiyo kushinda Kombe la
FA.
0 comments:
Post a Comment