Bodi ya Tumbaku nchini imevifuta vyama vyote vya wakulima
binafsi vya Tumbaku kwa madai kuwa vimekuwa vikisababisha kuwadidimiza wakulima
walioko katika vyama vya ushirika.
Akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wa Tumbaku kutoka
mikoa yote inayolima zao hilo,mweyekiti wa bodi ya Tumbaku nchini Said Nkumba
amesema imekuwepo tabia kwa vyama vya wakulima binafsi wa Tumbaku kuchukua
mikopo kwa kutumia mgongo wa wakulima walioko kwenye vyama vya ushirika na
baadaye kukiuka makubaliano kwa kuuza Tumbaku kwa kutumia vyama vyao huku
wakiwaacha wakulima wengine wakilipa madeni yaliyoachwa na wengine.
Wadau wa Tumbaku kwa upande wao wameitaka serikali kuwapa
kipaumbele wakulima wa zao hilo na kutambua mchango wake katika
kuiliingizia taifa fedha za Kigeni tofauti na mazao mengine sambamba na
kuangalia mfumo wa bei elekezi itakayokuwa na tija kwa wakulima ambao wamekuwa
wakipata shida katika kulima Tumbaku.
Mkutano wa wadau wa zao la Tumbaku umefanyika mkoani
Morogoro kwa kuwashirikisha wadau wa zao hilo na umejadili changamoto na
mafanikio yaliyopo katika uzalishaji wa zao hilo.
0 comments:
Post a Comment