Uchaguzi wa nafasi ya umeya katika jiji la Tanga umevurugika
baada ya madiwani kwa kushirikiana na viongozi wa chama cha wananchi CUF
kupinga matokeo yaliyotangazwa na msimamizi wa uchaguzi jimbo la Tanga wakidai
kuwa yamechakachuliwa hatua ambayo imesababisha askari kukabiliana na vurugu
hizo baada ya msimamizi kukimbia na kwenda kujifungia ofisini kwake kwa ili
kunusuru maisha yake.
Wakizungumza kwa jazba katika uchaguzi huo baadhi ya wafuasi
na viongozi wa chama cha wananchi CUF wamesema hawakubaliani na matokeo
hayo kwa sababu wapiga kura wa CUF walikuwa 20 na wale wa ccm ni 17 lakini katika
matokeo hayo msimamizi alitangaza kuwa mgombeanafasi ya umeya Selemani
Mustapher wa CCM amepata kura 19 na Hamad Rashid Jumbe amepata kura 18.
Wakielezea kwa masikitiko kuhusu mchakato wa uchaguzi huo
huku baadhi yao wakimwaga machozi baadhi ya wakereketwa wa CUF walioshiriki
kuwaapisha madiwani siku moja kabla ya uchaguzi ili wasiweze kurubuniwa
wamesema uchaguzi kama huo unaweza kusababisha maafa kwa sababu haukuwa wa haki
na kweli.
Hata hivyo mgombea nafasi ya umeya kwa tiketi ya CCM
Selemani Mustapher akizungumza katika zoezi hilo amewataka wananchi kuwa
watulivu na ameomba ushirikiano baada ya kutangazwa na msimamizi wa wa uchaguzi
jimbo la tanga Bwana Daud Mayeji.
0 comments:
Post a Comment