Katika siku za hivi karibuni,kumeibuka tabia ya baadhi ya
watu kutoa taarifa za uzushi na uongo kutumia majina ya taasisi,mashirika ya
umma na ofisi za Serikali na kueneza taarifa hizo katika mitandao ya
kijamii kwa lengo la kupotosha wananchi.
Miongoni mwa taarifa hizo ni pamoja na taarifa kuhusu Jeshi
la Polisi iliyosambazwa jana katika mitandao ya kijamii yenye kichwa cha
habari ‘chujio Jesho la polisi, vyeti feki vyawaonndoa askari kazini’ Taarifa
hiyo ni uzushi na hajatolewa na Jeshi la Polisi.
Kufutia hali hiyo, Jeshi la Polisi nchini linapenda
kukanusha taarifa hiyo ya uzushi ambayo haina ukweli wowote na inalengo
la kuchafua taswira ya Jeshi la Polisi kwa jamii.
Jeshi la Polisi nchini limeanza upelelezi wa kuwatafuta watu
wote waliohusika kueneza taarifa hiyo na kujifanya wao ni Jeshi la Polisi.
Aidha, Tunatoa onyo kali kwa watu wote kuacha kutumiamitandao ya kijamii
vibaya kwa kufanya uposhaji na badala yake watumia mitandao hiyo kwa
ajili ya ustawi wa jamii.
Imetolewa na:
Advera John Bulimba – SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya
Polisi.
0 comments:
Post a Comment