Image
Image

Breaking News.Ajali mbaya yahofiwa kuuwa na kujeruhi Tunduma.



Watu kadhaa wanasadikiwa kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa kufuatia Ajali iliyohusisha magari matatu yaani Coaster ya abiria iliyokuwa ikitokea Mbeya mjini kwenda Tunduma mjini,na Lori la Mafuta na Canter yakitokea Tunduma.
Kwa mujibu wa mashuhuda wanadai kuwa sababu na chanzo cha kutokea kwa ajali nikutokana na Lori la mafuta kujaribu kukwepa mwendesha Bajaji na Baiskeli katika eneo la Songea yalipo matuta ya shule ya Msingi ndipo ikatokea ajali.
Katika ajali hiyo inaelezwa kuwa abiria mmoja aliyejaribu kuruka kutoka kwenye Coaster aliangukiwa na Lori,dereva wa Coaster amejeruhiwa sana,abiria wengine wamepata maumivu ya hapa na pale.
Juhudi za kumtafuta kamanda wa Polisi mkoani humo zinaendelea ili kuthibitisha manusura wa ajali na waliopoteza maisha.



Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment