Image
Image

Rais Magufuli na Maalim Seif wakutana na kuzungumzia hali ya kisiasa Zanzibar.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo juu ya hali ya siasa ya Zanzibar na makamu wa kwanza wa rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Maalim Seif Sharifu Hamad Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Viongozi hao wawili wamekutana na kufanya mazungumzo hayo ikulu jijini Dar es Salaam kufuatia maombi ya Maalim Seif Sharif Hamad ya kutaka kukutana na rais Dr.John Pombe Magufuli na kufurahishwa na hali ya usalama na utulivu inayoendelea ambapo makamu huyo wa kwanza wa rais wa Zanzibar amemueleza rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli juu ya hali ya siasa ya Zanzibar kadri anavyoifahamu yeye.
kwa upande wake rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli amemshukuru Maalim Seif Sharif Hamad kwa taarifa kuhusiana na hali ya siasa Zanzibar na kumsihi waendelee na mazungumzo hadi suluhisho muafaka lipatikane.
Aidha viongozi hao wawili wamewaomba wananchi waendelee kuwa watulivu ili kutoa nafasi ya majadiliano yanayoendelea kufikia hatma njema na kuelezea matumaini yao kuwa vyama vya CCM na CUF haviwezi kushindwa kupata suluhu ya mgogoro huo.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment