Image
Image

Waumini wa dini ya Kiislamu na Kikristo nchini Kenya wameshambuliwa na Al Shabaab.



Baadhi  ya waumini wa dini ya Kiislamu na Kikristo  nchini Kenya wameshambuliwa  na kikundi cha Al Shabaab wakati wakisafiri kwa basi kutoka mji mkuu wa nchi hiyo Nairobi kuelekea eneo la Mandera.
Waumini hao walishambuliwa baada ya wapiganaji hao kulisimamisha basi na kuwataka wakae katika makundi mawili ya Wakristo na waislam ili waweze kuwaua wakristo kitendo ambacho kilipingwa na Waislamu ndipo shambulio hilo lilipotokea.
Katika tukio hilo ambalo limetokea eneo la Kaskazini Mashariki mwa Kenya karibu na mpaka na Somalia watu wawili waliuawa na wengine kujeruhiwa kufuatia kukaidi kwao kugawanyika kwa misingi ya dini.
Ikumbukwe  kuwa  mwezi april mwaka huu watu 148 waliawa kwenye chuo kikuu cha Garisa  kufuatia shambulio la kigaidi lililofanywa na wapiganaji hao wa Al Shabaab.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment