Image
Image

Uchaguzi wa wabunge na urais uliopangwa kufanyika jumapili hii nchini haiti umeahirishwa.


Uchaguzi wa wabunge na urais uliopangwa kufanyika jumapili hii nchini haiti umeahirishwa,baraza la muda la uchaguzi limetangaza katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jumatatu hii usiku. hakuna tarehe rasmi ambayo imetangazwa kufanyika kwa uchaguzi huu.
taarifa hii imekaribishwa na vyama vya wagombea wawili wa urais, jovenel moïse na jude célestin, lakini upinzani bado unaomba tume huru kuchunguza madai ya udanganyifu uligubika duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais.
kwa mujibu wa mwandishi wa rfi, katika mji wa port-au-prince, amélie baron, tangazo la jumatatu hii usiku la baraza la muda la uchaguzi (cep) la kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais na wabunge halikushangaza wengi. lilikuwa likisubiriwa na raia pamoja na vyama vya kiraia.
itafahamika kwamba mgombea wa upinzani, jude célestin, alikuwa bado hajatamka hadharani hata neno moja tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi. kuahirishwa kwa uchaguzi huo, kwa upande wake ni "hatua nzuri katika mwelekeo sahihi", lakini amesema jumatatu usiku kwamba alikuwa bado anasubiri "kuundwa kwa tume sahihi ya uchunguzi."
tume ya uchunguzi
jude célestin, mshirika wa karibu wa rais wa zamani réne préval, hapa anaikaba moja kwa moja serikali iliopo madarakani, akikanusha ufanisi wa tume iliyoundwa alhamisi iliyopita na michel martelly. tume ambayo hata hivyo ni dhaifu kwa sababu mmoja wa wajumbe wake bado anazusha masuali mengi kuhusu kazi anayopashwa kufanya.
katika kambi ya jovenel moïse, mgombea kwa tiketi ya utawala, tangazo la kuahirishwa kwa uchaguzi limepokelewa vizuri. grégory mayard paulo, mmoja wa wanasheria wa chama cha phtk chama, ametangaza kuwa angeweza "kuheshimu uamuzi wowote unaochukuliwa na cep".
sasa muda unayoyoma kwa kukamilisha uchaguzi huu nchini haiti kwani ufunguzi wa vikao vya bunge umepangwa januari 11 na rais mtarajiwa anapaswa kuanza shughuli zake tarehe 7 februari.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment