Image
Image

Polisi wa FFU aliyegushi vyeti atimka na asakwa.

JESHI la polisi mkoani Ruvuma, linamsaka askari wake wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) mwenye namba F,5425 PC Emmanuel Nyagol (35) anayedaiwa kutoroka kwa tuhuma za kugushi vyeti wakati akijiunga na jeshi hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji alisema askari huyo alitoroka Machi 16, mwaka huu .
Alisema inawezekana Nyagol amefikia uamuzi huo baada ya kuwapo tuhuma za kujiunga na jeshi hilo kwa kutumia  vyeti vya kughushi jambo ambalo ni kinyume cha taratibu za nchi.
Alisema  askari huyo aliajiriwa Aprili 28, mwaka 2003 na kupangiwa kituo cha kazi mkoani Ruvuma, baada ya kuhitimu mafunzo  mkoani Kilimanjaro.

Alisema askari huyo ametoroka na vitu vyake vya binafsi, kwani sare na  vitambulisho vyote ameviacha. Alisema jeshi hilo, linaendelea na msako dhidi ya PC Nyagol.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment