Image
Image

Rais Magufuli amtumbua Mkurugenzi Mtendaji TIC kwa kutochukua Mshahara wa Serikali tangu 2013.



Katika muendelezo wa utumbuaji majipu kwa watumishi wa Serikali ambao wanakua wanafanya kazi kinyume na miiko na maadili ya kazi katika serikali ya awamu ya tano iliyoingia na kasi ya aina yake hatimaye tena leo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli, ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha uwekezaji nchini (TIC),Bi.Juliet Kairuki kuanzia Aprili 24 mwaka huu.
Taarifa iliyotolewa na kwa vyo
mbo vya habari na katibu Mkuu wa Biashara na Uwekezaji,Prof. Adolf Mkenda,imesema kuwa hatua hiyo imekuja baada ya rais Magufuli kupata taarifa kuwa Mkurugenzi huyo alikua hachukui mshahara wa serikali tangu alipoajiriwa mwaka 2013 hatua ambayo imezua maswali mengi kwa Rais Magufuli.
Aidha Taarifa hiyo iliyosainiwa na Katibu Mkuu huyo imeongeza kuwa endapo Bi.Kairuki atakuwa tayari kuendelea kufanyakazi na Serikali ya awamu ya tano atapangiwa kazi nyingine huku mchakato wa kumpata Mkuregenzi mpya umeanza mara moja.
Kwa mujibu wa Prof. Mkenda kwenye taarifa yake hiyo amesema Bw.Clifford Katondo Tandali,atakaimu nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho cha uwekezaji nchini TIC.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment