Image
Image

Sakata la watumishi Hewa Mkuu wa wilaya ya Ukerewe awatumbua watumishi wawili wa Halmashauri.

                                              Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Joseph Mkirikiti.
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Joseph Mkirikiti, amewasimamisha kazi watumishi wawili wa halamshauri ya wilaya ya Ukwerewe, kwa tuhuma za ushiriki wa uwepo wa wafanyakazi hewa katika halmashauri hiyo.
Akizungumza na wakuu wa idara na watumishi wa halmashauri hiyo mjini Nansio Wilayani Ukerewe Mkirikiti amewataka watumishi hao kubadilika na kuacha kufanya kazi kwa mazoea jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo.
Mkirikiti amesema kuwa watumish iwanatakiwa kufanya kazi ambazo zitakua na tija kwa wananchi kwa kuondokana na mzigo wa matatizo yanayowakabili lakini sio kuhudhuria ofisini lakini unachofanya kwa wananchi hakionekani.
Akizungumzia suala la Watumishi waliohusika na uwepo wa wafanyakazi hewa ambao wameisababisha hasara serikali ameagiza katibu wa utumishi wa halmashauri na mtumishi wa idara ya utawala wa rasimali watu kusimamishwa kazi na vyombo vya dola vichukue hatua dhidi yao.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment