Image
Image

Mwigulu Nchemba: Nimewaelekeza polisi kuwashughulikia vinara wa vurugu na uchochezi

Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga aliyetaka kujua hatua ambayo serikali inachukua baada ya kubainika kuwa kuna wanasiasa wanahamasisha vurugu na uvunjifu wa amani, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Lameck Nchemba amesema kuwa Serikali haitavumilia kuona mtu ama kundi lolote likihatarisha amani na utulivu wa nchi kwa njia yoyote ile. Amesema kuwa kuna tabia imeanza kujitokeza kwa baadhi ya wanasiasa hasa wa vyama vya upinzani kutoa matamshi yenye kuchochea vurugu, uvunjifu wa amani na hata umwagaji damu. Amesema kuwa wizara yake kupitia Jeshi la Polisi itahakikisha kuwa vitendo hivyo vinakomeshwa mara moja ili nchi iemdeleee kuwa ya amani
" Mheshimiwa Naibu Spika, nimewaagiza vijana wangu ( polisi) kuwashughulikia wale tu vinara na si kuhangaika na wananchi wasio na hatia ambao wanapelekeshwa tu na wanasiasa hao. Amesema kuwa ipo tabia ya baadhi ya wanasiasa kutoa maneno ya uchochezi na kuwatanguliza wananchi wasio na hatia na pindi jeshi la polisi linapochukua hatua, wanaoathirika ni wananchi hao na si wale waliochochea. Kwa hali hiyo jeshi la polisi limeshabadili mbinu za kupambana na vitendo hivyo na badala yake itashugulika na wale vinara tu" Aliongeza Waziri.
Mytake: Niwapongeze Jeshi la Polisi na Wizara ya Mambo ya ndani kwa kuliona hili. Hii ndio njia muafaka ya kuwatulia hawa wahalifu bila ya kuleta madhara. Naona kazi imeshaanza hasa kwa kuwaita na kuwahoji baadhi ya wanasiasa wa upinzani akiwemo Mbowe, Tundu Lissu, Zitto Kabwe, Ole Sosopi, Kubenea nk. Kazi imeshaanza. Heshima inarudi.
sOURCE:JF.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment