Image
Image

Wabunge watatu wa upinzani wasimamishwa kutohudhuria vikao vya bunge kwa wakati tofauti.

Bunge limeazimia kuwa mbunge wa Mbeya Mh.Joseph Osmond Mbilinyi asimamishwe kuhudhuria vikao 10 vya bunge la 11 kuanzia kikao cha leo Juni 30 mpaka hapo adhabu itakapokuwa imekamilika. Bunge limepitisha kwa kauli moja adhabu hiyo.
Joseph Mbilinyi (Mb) amekiri kunyoosha kidole cha kati juu wakati akitoka bungeni baada ya kusika mbunge amemtusi mama yake. Mh. Mbilinyi amejitetea kuwa ni kweli alinyoosha kidole cha kati juu baada ya kumsikia mbunge wa CCM akimtusi mama yake mzazi hivyo kupata short temper na kujikuta akitenda kosa hilo.
Pia Joseph Mbilinyi amesema kuwa alinyoosha kidole cha kati juu kama kupinga kile kilichokuwa kinafanyika na mbunge huyo wa CCM, alipoulizwa na Kamati ya Maadili inayoongozwa na Mh. Mkuchika, Mh. Mbilinyi alisema kuwa kunyoosha kidole cha kati juu hakina maana ya moja kwa moja hivyo kwa uelewa wake yeye alikuwa anapinga kitendo cha mbunge wa CCM.
Kamati ya maadili imeridhika kuwa kitendo cha Joseph Mbilinyi (Mb) kuonesha kidole cha kati juu ni kosa na kutoheshimu mamlaka ya Spika wa bunge baada ya kupitia matoleo ya maana mbalimbali ya (Kuonesha kidole cha kati juu) nchi tofauti tofauti.


Katika hatua nyingine pia Mbunge wa Simanjiro James Millya amesimamishwa kutohudhuria vikao vitano vya Bunge kwa kusema uongo Bungeni na Mhe.Said Kubenea 

kutohudhuria vikao vitano vya Bunge kutokana na kushindwa kuthibitisha kauli alizotoa bungeni kuwa kampuni ya ujenzi imeingia mkataba wa kujenga nyumba za jeshi pamoja ba nyumba moja waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa,Mhe Dkt Hussein Mwinyi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment