Image
Image

Wabunge wa Upinzani Tanzania waandamana kupinga ukiukwaji wa Demokrasia.

Wabunge wa vyama vya upinzani nchini Tanzania hivi leo Bungeni mjini Dodoma wamebuni aina mpya ya kufikisha ujumbe kwa kiti cha Spika na kwa watanzania kwa kuvalia mavazi Meusi na Mabango yenye ujumbe mbalimbali.
Wabunge hao ambao wamesusia vikao vya bunge kwa muda sasa kwa kile wanachopinga Naibu Spika Tulia Ackson kuendesha kinyume na Taratibu za kiti hicho wamesema kutoka kwao huko bungeni ni kupinga  ukiukwaji wa Demokrasia ndani ya Bunge na kuahidi kufikisha ujumbe huo kwa wananchi mara baada ya kuahirishwa Bunge.
Mwenyekiti mwenza wa UKAWA Mhe. James Mbatia amebainisha kwamba kutoka kwao Bungeni wanaelewa wanachokifanya kwa kuwa wametumwa na wananchi kuwawakilisha hivyo hawapo tayari kuona haki yao ikiporwa.
“Tumewawakilisha watanzania waliotutuma kuja ndani ya Bunge hili, tuna akili timamu, tukitoka hapa sasa chuki tuliyonayo na hasira tunazipeleka ndani ya jamii ya watanzania, kueleza namna haki yao inavyoporwa”Amesema Mbatia.
Wakiwa wameongozana kwa pamoja huku wakiwa wamevalia mavazi hayo meusi na kubeba Mabango hayo Meupe yenye maandishi Meusi yamesindikizwa na wimbo wa Solidarity Forever
ambao umekuwa wimbo unaoimbwa mara kadhaa na wafanyakzi kutoka taasisi,mashirika,vyama vya wafanyakazi nk.kwa kuhamasisha umoja na mshikamano kama wanataifa moja pale ambapo wanaona hawasikilizi ama hawasikilizani katika jambo linalohitaji mashauriano ili kutatua jambo lenye mkwamo ndani ama nje ya Taifa.
Kwa siku kadhaa wabunge hao walifanya tena staili mpya ya kufikisha ujumbe kwa wanachoonekana kuchoshwa na kiti cha Naibu Spika,kwa kuziba midomo yao kwa Plasta nyeupe na kutoka ndani ya bunge ikiwa nimuendelezo wa kususia vikao hivyo mara tu naibu huyo atakapokuwa akiongoza.
Wabunge hao wa upinzani wamekuwa wakionekana tu pale kwenye sala ya kufungua Bunge nakisha sala inapoisha hutoka nje na kuendelea na shughuli zao.
Kwa siku ya 22 June, nao Wabunge wa Chama cha Democrat cha Marekani waliligomea Bunge kukaa kwenye viti na kuamua kukaa chini kushinikiza kutungwa kwa sheria ya kudhibiti umiliki wa bunduki.
Tupe maoni yako hapa na Like Page yetu ya Facebook hapo.




Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment