Image
Image

Maelfu ya waombolezaji na viongozi wa kimataifa wamzika Rais wa zamani wa nchi hiyo Shimon Peres.

Maelfu ya waombolezaji na viongozi wa kimataifa walikusanyika Israel kumzika Rais wa zamani wa nchi hiyo Shimon Peres ambaye alitajwa kama kiongozi aliyechangia katika juhudi za amani Mashariki ya Kati.
Ni mazishi yaliohudhuruwa na viongozi mbali mbali wa kimataifa huku rais Barrack Obama wa Marekani na aliyekuwa rais wa nchi hiyo Bill Clinton pamoja na rais wa Palestina Mahmoud Abbas wakiongoza orodha kubwa ya viongozi hao wa kimataifa waliokongamana katika eneo la makaburi ya kitaifa  nchini Israel la mlima Herzl kwa mazishi hayo.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa ujumbe huo wa viongozi mbali mbali wa kimataifa ni ishara ya  wazi ya upendo aliokuwa nao Shimon Peres, matumaini na kiu cha amani na mapenzi kwa nchi yake Israel. Alikuwa mtu aliyependwa na Israel na aliyependwa pia na ulimwengu aliongeza kusema Benjamin Netanyahu. "Leo ninakulilia. Nilikupenda, sote tulikupenda. Kwaheri Shimon, mtu mzuri, kiongozi mashuhuri. Tutakuweka ndani ya moyo wa taifa letu na ninachukua nafasi hii kusema kuwa utakumbukwa katika mioyo ya mataifa yote," alisema Netanyahu.
Rais Barack Obama aliyekuwa na uhusiano wa karibu na marehemu Peres, alisema kuwa hakuna kiongozi aliyetekeleza mengi zaidi ya Peres katika kuimarisha uhusiano kati ya Marekani na Israel. Kadhalika Obama ametilia mkazo suala la amani akisema kuwepo katika maziko hayo, rais wa mamlaka ya Wapalestina kunaonesha haja ya kuliangalia suala la amani Mashariki ya Kati. "Ni hesima kubwa kwangu kuwa Jerusalem kumuaga rafiki yangu Shimon Peres, aliyetuonyesha kuwa haki na matumaini ndiyo kiini cha maadili ya Kiyahudi."
Kiongozi aliyeshika vyeo vingi
Bill Clinton alimtaja Peres kuwa mtu aliyekuwa na ndoto kubwa. Aliongeza kuwa Peres alianza kwa kuwa mwanafunzi mwerevu zaidi nchini Israel, mwalimu bora zaidi na hatimaye kumalizia kwa kuwa mwenye maono makubwa kwa taifa la Israel na kwamba aliishi maisha yake ya miaka 93 kufikiria jinsi kila mmoja alivyoweza kutumia uwezo wake kikamilifu na kwamba watu wanapaswa kujiepusha na hofu na kuishi kila siku kikamilifu huku kukiwa na matumaini ya kesho.
Watoto wa Peres pia walimtaja baba yao kama mtu aliyekuwa na upendo kwa familia yake. Bintiye Tzvia Walden alisema kuwa babake alipenda kujifunza mambo mbali mbali na kupata elimu mpya kila mara .
Mwanawe wa kiume alichekesha waombolezaji aliposema kuwa wakati babake alipowahi kuulizwa angetaka aandikiwe ujumbe gani juu ya kaburi lake, babake alimjibu kuwa yeye ni mchanga sana kufariki.
Peres aliwahi kuwa Rais, Waziri Mkuu na waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wakati wa  uhai wake katika safari yake ya  kisiasa.
Alifariki  mapema wiki akiwa na umri na umri wa miaka 93 kutokana na ugonjwa wa kiarusi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment