Image
Image

Ufisadi wamuweka matatani Waziri mkuu wa zamani wa Israel.

Mahakama kuu ya Israel imekataa ombi la dhamana lililowasilishwa na waziri mkuu wa zamani Ehud Olmert aliyekutwa na hatia ya kuhusika na ufisadi.Kulingana na taarifa za kituo cha redio cha Israel, iliarifiwa kwamba Olmert ameongezewa miezi 8 zaidi kwenye hukumu ya kifungo cha miezi 19 aliyopewa hapo awali na mahakama.
Kufuatia uamuzi wa mahakama kuu wa kukataa dhamana, Olmert atalazimika kutumikia kifungo cha miaka 2 na miezi 3 gerezani.
Baada ya kukabiliwa na kashfa ya ufisadi, Olmert alitupwa gerezani na kuanza kutumikia kifungo cha miezi 19 tangu mwezi Februari mwaka huu.
Kesi hiyo iliibuka baada ya Olmert kudaiwa kupokea rushwa kwa ajili ya mradi wa Holyland Park wakati alipokuwa akihudumu kama meya wa manispaa ya mji wa Jerusalem.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment