Image
Image

Serikali za Uganda na Tanzania zawekeana mkataba wa pamoja wa mradi wa bomba la mafuta ghafi.

Serikali za Uganda na Tanzania zimewekeana mkataba wa pamoja wa mradi wa bomba la mafuta ghafi wa nchi za Afrika Mashariki litakalojengwa kwa ushirikiano baina ya nchi hizo mbili na wawekezaji wa kimataifa unaokadiriwa kufikia zaidi ya dola za kimarekani bilioni 3.5.
Mkataba huo umefanyika jijini Tanga na kuhudhuriwa na mashirika ya kimataifa, mabalozi wa nchi za umoja wa ulaya, viongozi wa serikali ya Tanzania na Uganda ambapo katika mchakato huo waziri wa nishati na madini wa Tanzania Profesa Sosypeter Muhongo na waziri mwenzake wa Uganda Irine Muloni wamewahakikishia wananchi kuwa mradi huo utaimarika na kukamilika mwaka 2020.
Naye waziri wa mafuta wa jamhuri ya kidemkrasia ya Congo Profesa Aime Mukena amewataka wafanyabishara wa Tanzania hasa wanaojihusisha na mafuta kwenda kuwekeza katika nchi yao kufuatia changamoto ya uhaba wa bohari za mafuta zinazoikabili baadhi ya mikoa katika taifa la Congo.
Kufuatia hatua hiyo baadhi ya wawekezaji wa nishati na madini nchini wameihakikishia serikali ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kuwa wameanza kusaidia nchini kuongeza hifadhi za mafuta huku wakiendelea na bomba la mafuta kutoka Uganda kuja jijini Tanga.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment