Image
Image

Mwijage:Tanzania imeweka mazingira bora ya uwekezaji.

WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, amesema Tanzania imeweka mazingira bora ya uwekezaji wa biashara kupitia Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC). Akizungumza katika mkutano kati ya wafanyabiashara wa Tanzania na Ubelgiji, jijini Dar es Salaam jana, Mwijage alisema kuwa mazingira yaliyowekwa ni rafiki kwa uwekezaji katika maeneo mbalimbali ikiwemo ya kilimo cha biashara.
Mwijage alisema kuwa Tanzania ni nchi inayokua kwa kasi duniani hivyo wawekezaji wana nafasi ya kufanya uwekezaji kutokana na kuwa nchi ya amani ambapo wanaweza kuwekeza na kuzalisha bila kuwepo kwa vikwazo.
Alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inapambana na rushwa ili wananchi waishi bila rushwa, na kuyataja maeneo ya kufanya uwekezaji yamepangwa katika maeneo ya biashara, kilimo, miundombinu, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), madini, gesi, utalii na uvuvi.
Alisema kuna ushirikiano wa muda mrefu kati Tanzania na Ubelgiji hivyo milango ya uwekezaji iko wazi na nchi nyingine zimeweka mikakati ya uwekezaji.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment