Image
Image

ZFA yamtia kitanzi cha miezi 6 Mwamuzi kutochezesha soka.

CHAMA cha Soka Zanzibar (ZFA) Taifa kimemfungia mwamuzi Rashid Farahani Webu kuchezesha mpira wa miguu kwa kipindi cha miezi sita kutokana na kitendo chake cha kushindwa kuzitafsiri kanuni zinazohusika na uchezeshwaji wa mchezo huo. Kwa mujibu wa barua ya chama hicho iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari, mwamuzi huyo alifanya kitendo hicho wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar Kanda ya Unguja kati ya Miembeni na Jang’ombe Boys baada ya kutoa maamuzi yaliyokinzana na kuandika ripoti isiyosahihi.
Barua hiyo ambayo imetiwa saini na Makamu wa Rais wa ZFA Unguja, Mzee Zam Ali inaeleza kwamba uamuzi huo umetokana na kifungu cha 25(d) cha kuendeshea mpira wa miguu Zanzibar.
“ZFA inakufungia kuchezesha mpira wa miguu kwa kipindi cha miezi sita kwa kushindwa kuzitafsiri vyema kanuni zinazohusika na uchezeshwaji wa mchezo huo, kitendo ambacho kilikufanya kutoa maamuzi yasiyoshihi, “ilisema sehemu ya barua hiyo.
Sambamba na kufungiwa mwamuzi huyo pia alitakiwa kwa kipindi chote hicho cha kutumikia adhabu yake kuhudhuria masomo yanayoandaliwa na Kamati ya Waamuzi, ili aweze kupata uelewa mzuri.
Katika hatua nyingine wachezaji wanne wa timu ya Kimbunga wamefungiwa kucheza mpira ndani na nje ya Zanzibar kuanzia tarehe ya barua hiyo hadi mwisho wa msimu wa ligi 2017/2018 kutokana na kitendo cha kufanya vurugu na vitendo vinavyokwenda kinyume na maadili ya uanamichezo.
Wachezaji hao ni Haji Nahoda Haji, Shomari Waziri Ali, Juma Simai Shukuru na Idrissa Simai Pandu ambao bila ya uhalali wowote wanadaiwa kumpiga mwamuzi Ramadhan Kessy aliyechezesha kati yao na timu ya KMKM kwenye Uwanja wa Fuoni, ambao ulivunjika katika dakika ya 26.
Adhabu hiyo kwa wachezaji hao imetolewa chini ya vifungu vya 26c(ii) na 26c(iii) vya kuendesha na kuchezesha soka katika Ligi Kuu ya Zanzibar 2016/2014.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment