Image
Image

IGP Sirro, atuma salamu kwa wauaji wa Rufiji, Ikwiriri na Kibiti asema mwisho wao umefika.

Mkuu wa Jeshi la polisi chini Tanzania IGP Simon Sirro ametuma salamu kwa wahalifu ambao wamekuwa wakifanya mauaji Rufiji, Ikwiriri na Kibiti mkoani Pwani kwamba sasa muda wao umekwisha wakufanya vitendo hivyo na kuahidi kuwa yeyote atakaye fanikisha kukamatwa kwa wahalifu hao atapatiwa kiasi cha shilingi milioni 10.
"Niwahakikishie watanzania kwamba suala la Rufiji, Ikwiriri na Kibiti ni suala la muda mfupi, viongozi wangu wamezungumza, Mh.Rais amezungumza, Waziri wa Mambo ya Ndani ameznungumza, mimi sitaki kulizungumzia tena ninacho sema watanzania wanataka kupata majibu"Amesema IGP Sirro.
IGP Sirro amesisitiza kwamba yeye pamoja na jeshi la polisi pamoja na vyombo vingine vya dola nilazima watapata majibu ya kinaga ubaga dhidi ya wauji wa rufiji.
"Mimi niwape tu salamu kile kikundi cha watu wachache, wawe ni watanzania hawana sababu ya kuwafanyia watanzania wenzao ubaya, lakini siku zote wanasema mwenzako akikufanyia ubaya huna sababu ya kufanya ubaya, lakini waandishi wa habari kwa hao wanaofanya ubaya tupeleke tu salamu kwamba ubaya huu tutajibu kwa ubaya kwa mujibu wa Sheria"Amesema IGP Sirro.
Sirro amesema majibu ya Rufiji, Ikwiriri na Kibiti hayatachukua muda mrefu katika kuwashughulikia ili wananchi wa maeneo hayo waishi kwa amani na utulivu.
Katika hatua nyingine IGP Simon Sirro amewaonya askari wa Jeshi hilo wanao pokea rushwa kuacha mara moja na atakaye bainika atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kufukuzwa kazi na kuburuzwa Mahakamani.
IGP Sirro vile vile amewataka wananchi ambao wanapenda kuwashawishi askari kuchukua rushwa kuacha kwani atakaye bainika pia atapata adhabu ya kufanya kitendo hicho ambacho ni kinyume cha sheria na taratibu, kwani rushwa ni adui ya haki. 
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment