Image
Image

TANZIA:Mzee Ngosha aliyechora Nembo ya Taifa ya Adam na Hawa afariki.


Mzee Francis Maige Kanyasu(Ngosha) enzi za uhai wake, akiwa amelazwa Wodi ya Mwaisela katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu ya maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.
Dar es Salaam.
Mbunifu wa Nembo ya Taifa  ya Adam na Hawa, iliyotumika kitaifa nchini Tanzania , Mzee Francis Maige (Ngosha) aliyekuwa akipatiwa Matibabu katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Ngosha aliyepelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wiki iliyopita kwa ajili ya matibabu, amefariki dunia saa 2 usiku Mei 29.
Taarifa iliyotolewa na uongozi wa Hospitali ya Muhimbili imeeleza kuwa hali ya Ngosha ilibadilika ghafla akiwa hospitali hapo.
“Mwili wake umehifadhiwa katika chumba cha maiti hapa Muhimbili na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa na mamlaka husika.” imesema taarifa hiyo.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment