Image
Image

Upadates Kutoka Kituo cha Polisi Chang'ombe anaposhikiliwa kiongozi wa ACT Wazalendo.

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu Zitto Kabwe, amekamatwa na polisi na kuhojiwa akituhumiwa kufanya makosa ya Uchochezi.
Kwamba juzi, Oktoba 29, 2017 alipokuwa kwenye mkutano wa kuzindua kampeni za udiwani katika Kata ya Kijichi, Wilayani Temeke alitoa maneno yanayoweza kupelekea uvunjifu wa amani. Maneno hayo ni yafuatayo:
1. Kwamba wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kufanya uchunguzi na kuwakamata watu waliompiga risasi Mbunge Tundu Lissu mpaka siku hiyo.2. Kwamba wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kueleza chanzo cha miili ya watu wanaookotwa kwenye fukwe za bahari kama Coco Beach. Hivyo kuichagua CCM ni sawa na kuwaunga mkono waliofanya vitendo vya kumshambulia Tundu Lissu na wanaoua watu wanaookotwa kwenye fukwe.
Timu ya mawakili wa chama iko na ndugu Zitto katika mahojiano haya.
Kamati ya Sheria na Katiba
ACT Wazalendo 
Oktoba 31, 2017
Dar es salaam
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment