Image
Image

VIGOGO sita wa TANESCO wamepandishwa kizimbani Kisutu.

VIGOGO sita wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka 202, likiwemo la kula njama na kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 2.7.
Washitakiwa hao ni Emillian Mlowe, Bashiru Ngela, Barnabas Masaby, Shakira Ngela, Mkama Maira na Yared Jonas. Akisoma mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi, Victoria Nongwa, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi alidai kuwa Januari 7 mwaka 2014 na Januari 31, mwaka 2015 maeneo ya Dar es Salaam, walikula njama ya kutenda kosa la wizi.
Wakili Kishenyi alidai katika mashitaka ya pili, mshitakiwa Mlowe, Ngela, Maira na Jonas katika maeneo ya Tanesco Kinondoni, Dar es Salaam, wakiwa waajiriwa wa nafasi za uhasibu, walikuwa na uwezo wa kuingia katika mfumo wa kompyuta kwa njia ya ulaghai walifanya maingizo ya uongo kuonesha kwamba Sh 2,746,485,545 zililipwa kwa Tanesco kama manunuzi ya umeme.
Katika mashitaka ya tatu hadi 201, washitakiwa wote kwa pamoja katika tarehe tofauti waliiba mamilioni ya fedha kupitia mfumo huo. Wakili wa serikali, Gloria Mwenda alidai kati ya Julai Mosi, 2014 na Machi Mosi, mwaka huu, maeneo ya Tanesco Kinondoni washitakiwa walisababisha hasara ya Sh 2,746,485,545 ambazo walionesha zimelipwa na wakala wa Tanesco wakati wakijua ni uongo.
Upande wa waendesha mashitaka ulidai upelelezi wa shauri hilo haujakamilika. Hata hivyo, hakimu Nongwa alisema washitakiwa hawatakiwi kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza mashitaka ya uhujumu uchumi.
Pia alisema mahakama haiwezi kutoa dhamana kwa sababu thamani iliyotajwa ni zaidi ya Sh milioni 10, hivyo wanapaswa kuomba dhamana Mahakama Kuu. Alisema washitakiwa warudishwe rumande hadi Novemba 21 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na kuutaka upande wa mashitaka kukamilisha upelelezi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment